Sonship Stories

Swahili Stories

Yesu na Mafarisayo: Mabishano ya Sabato

Marko 2:28-3:6

Mandhari Muhimu: Matumizi ya sheria; kujihesabia haki

[Dhana Muhimu za Injili: Matumizi ya Sheria]

Siku moja ya Sabato, Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakipita katika mashamba ya nafaka, na wanafunzi wake walipokuwa wakitembea wakaanza kukwanyua masuke ili kula. Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, kwa nini wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya sabato?”

Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma alivyofanya Daudi, wakati yeye na wenzake walipokuwa na njaa na wanahitaji? Katika siku za Abiathari, kuhani mkuu, Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, akala ile mikate mitakatifu, ambayo ni halali kwa makuhani peke yao kula, akawapa na wenzake pia."

Yesu akawaambia Mafarisayo, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato, kwa hiyo Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa sabato.

Wakati mwingine Yesu aliingia katika sinagogi, na mle palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza. Kwa kuwa ilikuwa siku ya Sabato, baadhi ya Mafarisayo walikuwa pale, wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, hivyo wakamwangalia sana waone kama atamponya mtu huyu, ndipo wapate kumshtaki kwamba alifanya kazi siku ya Sabato.

Yesu akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, "Simama mbele ya watu wote." Na mtu huyo alifanya. Ndipo Yesu akawauliza Mafarisayo, ni ipi iliyo halali siku ya sabato, kutenda mema au mabaya, kuokoa maisha au kuua? Lakini walikaa kimya na hawakujibu.

Naye Yesu akawatazama pande zote kwa hasira, akihuzunishwa na ugumu wa mioyo yao. Yesu akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Nyosha mkono wako. Yule mtu akafanya, na mkono wake ukapona kabisa.

Kisha Mafarisayo wakatoka na kuanza kufanya njama pamoja na wafuasi wa Herode jinsi ya kumwua Yesu.

 

AYA ya KUKUMBUSHA: Mark 2:27,28 Then he said to them, “The Sabbath was made for man, not man for the Sabbath. So the Son of Man is Lord even of the Sabbath.”