Sonship Stories

Swahili Stories

Yesu na Kijana Tajiri

Matayo 19:16-26 (& Luka 18:18-30, Marko 10:17-27)

MADA MUHIMU: Kujitegemea, Imani, matumizi ya Sheria

[Dhana Muhimu za Injili:Imani, Matumizi ya Sheria, Kuhesabiwa Haki]

Siku moja, kijana tajiri aliyekuwa pia kiongozi alimjia Yesu na kumwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mimi mwema? Hakuna aliye mwema ila Mmoja tu, ndiye Mungu: Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”

Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?”

Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.”

Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” Yesu alimtazama na kumpenda. Akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu,

nenda, kauze vitu vyote ulivyo navyo na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Amin, amin nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana.”

 

AYA wa KUKUMBUSHA: Mathayo 19:26: “Kwa wanadamu hilo [i.e., kuokoka] haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.