Utambulisho katika Kristo,
MADA MUHIMU: Ibada ya Sanamu
Shadraka, Meshaki, na Abednego walikuwa marafiki wa karibu wa Danieli na walikuwa Waisraeli walioishi uhamishoni Babiloni. Walikuwa wakimfuata Bwana kwa uaminifu na wakuwa na vyeo vya juu katika serikali ya Babeloni.
Basi ikawa Mfalme Nebukadreza alitengeneza sanamu ya dhahabu yenye urefu wa mita thelathini na kuisimamisha katika tambarare ya Babeli. Kisha akawaita viongozi wote wa Babeli waje kwenye kuwekwa wakfu kwa sanamu aliyokuwa ameisimamisha. Wakaja wote na kusimama mbele yake, na mtangazaji akapaaza sauti, akisema, “Hili ndilo jambo mliloagizwa kufanya, enyi watu wa kabila zote, na mataifa, na watu wa lugha zote: Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta na gitaa na filimbi na vyombo vya muziki vya aina zote, mnapaswa kuanguka chini na kuiabudu sanamu ya dhahabu ambayo mfalme Nebukadreza ameisimamisha. Yeyote ambaye hataanguka chini na kuabudu atatupwa mara moja katika tanuru inayowaka moto.” Kwa hiyo, mara tu waliposikia sauti mbalimbali za muziki, watu wote walianguka chini na kuiabudu sanamu hiyo.
Kulikuwa na watu wengine waliowachukia Wayahudi na walikuwa na wivu kwa Shadraka, Meshaki, na Abednego, kwa hivyo walimwambia mfalme kwamba hawa watatu walikataa kumsikiliza mfalme, kuitumikia miungu yake au kuiabudu sanamu ya dhahabu aliyokuwa ameisimamisha.”
Ndipo Nebukadreza akakasirika sana, akawaita Shadraka, Meshaki, na Abednego, akawaambia, “Je, ni kweli kwamba mnakataa kuitumikia miungu yangu na kuiabudu sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi, nitawapatia nafasi nyingine moja tu! Sasa mtakaposikia sauti za aina zote za muziki, mkiwa tayari kuinama na kuiabudu sanamu niliyoifanya, ni vyema sana. Lakini msipoiabudu, mtatupwa mara moja katika tanuru inayowaka moto. Basi ni mungu gani atakayeweza kuwaokoa ninyi kutoka mkononi mwangu?”
Shadraka, Meshaki na Abednego wakamjibu mfalme, “Ee Nebukadreza, hatuhitaji kujitetea mbele yako katika jambo hili. Tukitupwa ndani ya tanuru
hiyo inayowaka moto, Mungu tunayemtumikia aweza kutuokoa kutoka humo, naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Lakini hata asipofanya hivyo, tunataka ujue, Ee mfalme, kwamba sisi hatutakubali kuitumikia miungu yako, wala hatutaisujudia sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, Meshaki, na Abednego. Akaamuru tanuru iwashwe moto mara saba kuliko kawaida, akaamuru baadhi ya askari hodari kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kamba na kuwatupa ndani ya tanuru ile wakiwa wamevaa nguo zote. Kwa hiyo, kwa sababu tanuru ilikuwa na moto sana, askari waliowatupa waliuawa wenyewe.
Ndipo mfalme Nebukadreza akaruka kwa miguu yake kwa mshangao na kuwauliza washauri wake, “Je, hatukuwa na watu watatu ambao tuliwatupa motoni? Tazama! Ninaona watu wanne wakizunguka motoni, bila kufungwa wala kujeruhiwa, na wa nne anafanana na mwana wa miungu.” Nebukadreza akakaribia mlango wa tanuru yenye moto na kupaaza sauti, “Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Zaidi, tokeni nje! Njoo hapa!"
Kwa hiyo Shadraka, Meshaki na Abednego wakatoka nje ya moto, na Nebukadreza na washauri wake wakawazunguka. Waliona ya kuwa moto haukuwadhuru miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea; mavazi yao hayakuungua, wala hapakuwa na harufu ya moto juu yao.
Kisha Nebukadreza akasema, “Asifiwe Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake! Walimwamini na kukaidi amri ya mfalme na walikuwa tayari kutoa maisha yao badala ya kumtumikia au kumwabudu mungu yeyote isipokuwa Mungu wao wenyewe. Kwa hiyo ninaamuru kwamba watu wa taifa lolote au lugha yoyote wanaosema neno lolote dhidi ya Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abednego waangamizwe kabisa, kwa maana hakuna mungu mwingine awezaye kuokoa kwa njia hii.” Ndipo mfalme akawapa vyeo Shadraka, Meshaki na Abednego katika wilaya ya Babeli.
Optional Memory Verse: Kutoka 20:2-5a: “Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu…”