Sonship Stories

Swahili Stories

Mwito wa Isaya

Isaya 6:1-13; 2 Mambo ya Nyakati 26 (Usuli: 2 Mambo ya Nyakati 26:1-23)

MADA MUHIMU: Utakatifu wa Mungu na Dhambi wa Mwanadamu;

Matumizi Sahihi ya Sheria

[Dhana Muhimu za Injili: Matumizi ya Sheria, Dhambi, Kuhesabiwa Haki, Haki Inayopokelewa, Toba]

Usuli wa Hadithi:

Uzia alikuwa mmoja wa wafalme wema wa Yuda wakati wa ufalme uliogawanyika. Kadiri alivyomtafuta Bwana kwa unyenyekevu na kuwasikiliza makuhani wa Bwana, Mungu alimpa Uzia

mafanikio dhidi ya adui zake. Lakini baadaye alijivuna na kujaribu kufanya kazi ya makuhani kufukiza uvumba Hekaluni, akipuuza kilio cha makuhani cha kumtaka asimame na kuondoka. Kwa hiyo Bwana akampiga na ugonjwa wa ukoma, naye akafa peke yake, asiweze kwenda tena hekaluni. Isaya alikuwa

mmoja wa manabii wakuu ambao Mungu aliwatuma kwa Yuda ili kuwaonya juu ya hukumu kwa ajili ya dhambi zao, na kuwapa tumaini la baraka za wakati ujao watakapotubu. Hii ni hadithi ya jinsi Mungu

alivyomwita Isaya wakati wa huzuni baada ya Uzia kufa akiwa na ukoma. Isaya anaandika anaeleza kilichotokea. Alisema

 

“Katika mwaka Mfalme Uzia alikufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi. Naye alikuwa juu akatukuzwa pia. Joho lake (kanzu yake) likajaza hekalu. Juu yake walikuwepo malaika wengi, kilammoja alikuwa na mabawa sita: kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana Mwenye nguvu, dunia yote imejaa utukufu wake.” Kwa kutoa kwao sauti, mahali pale pote palitikisika, na hekalu likajaa moshi.

Isaya akalia, “Ole wangu mimi nimeangamia! Kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu.”

Ndipo mmoja wa wale malaika akaruka kunijia akiwa na kaa la moto linalowaka mkononi mwake, ambalo alikuwa amelichukua kwa koleo kutoka madhabahuni.

Akanigusa kinywa changu na kusema, “Tazama, hili limegusa midomo yako; hatia yako imeondolewa, na dhambi yako imepatanishwa.”

Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Nami nikasema, ‘‘Mimi hapa. Nitume mimi!”

Halafu Mungu akampatia Isaya kazi ngumu sana ya kuenda na kuhubiria watu wa mioyo migumu ambao wachache tu wanaweza kupokea ujumbe. Wachache watatubu na kumwamini Mungu.

 

AYA ya KUKUMBUSHA: Zaburi 51:1-3: “Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako., uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu. Na dhambi yangu i mbele yangu daima.”