MADA MUHIMU: Kujihesabia haki, Unyenyekevu, Toba, Matumizi ya Sheria
[Dhana Muhimu za Injili: Dhambi, Toba, Matumizi ya Sheria, Kuhesabiwa Haki]
Siku moja Yesu alitoa mfano huu kwa wale walijiona kuwa wao ni wenye haki na huwadharau wengine.
“Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. Yule farisayo, alikuwa amesimama pekee yake, akasali hivi: ‘Mungu, ninakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine; wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma, natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu’
Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipiga kifuani na kusema, ‘Mungu nihurumie, mimi mwenye dhambi’
“Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa na yeyote ajishushaye atakwezwa.”
AYA ya KUKUMBUSHA: Waebrania 10:19-22: “Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajilii yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili Wake, basi kwakuwa tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyuziwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya…”