Sonship Stories

Swahili Stories

Maria na Martha

Luka 10:38-42, Mwanzo 3

Mada Muhimu: Ushirika na Bab

[Dhana Muhimu za Injili: Urafiki wa karibu na Baba, Dhambi, Utambulisho katika Kristo]

Siku moja Yesu na wafuasi wake walikuwa wakisafiri, na wakafika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake. Martha alikuwa na dada yake aliyeitwa Maria. Maria aliketi chini miguuni mwa Yesu akisikiliza yale aliyokuwa akisema. Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha kaja kwa Yesu akamuuliza, “Bwana, hujali kwamba dada yangu ameniachia kazi yote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie!”

Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna atakaye mwondolea”

 

AYA ya KUKUMBUSHA: Luka 10:42: “Kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna atakayemwondolea.”