Sonship Stories

Swahili Stories

Abramu -Imani Kuhesabiwa Haki

Mwanzo 12:1-8; Mwanzo 15

MADA MUHIMU: Kuhesabiwa Haki kwa Imani, Kuishi kwa Imani, Utambulisho katika Kristo

Baada ya siku za Nuhu na Mnara wa Babeli, kulikuwa na mtu mmoja aliteitwa Abramu. Alikuwa na umri wa miaka 75, mke wake, sarai, alikuwa mkongwe pia, na hawakuwa na watoto. Siku moja, Mungu alimtokea abramu na akamwambia “Abramu, ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uuende mpaka nchi nitakayokuonyeha. Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, nitalikuza jina lako, nawe utakuwa Baraka, nitabariki wale wanaokubariki, ye yote akulaaniye nitamlaani na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa”

Abrahamu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, wakasafiri mpaka nchi ya Kanani. Huko Mungu akamtokea akamwambia “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Wakati huo kulikuwa na njaa katika nchi. Kwa hiyo Abramu akaichukua familia yake mpaka Misri. Huko, ingawa Abramu alitenda dhambi kwa kutomwamini Bwana na kusema uongo kwa mfalme, Mungu, kwa huruma yake, alimlinda yeye na familia yake, kutoka kwa njaa na kutoka kwa Wamisri na hata akambariki Abramu kwa mali nyingi wakati huo.

Abramu na familia yake waliporudi kanani kutoka Misri, walikuwa na wanyama wengi. Wote wawili, Abramu na Loti, walikuwa matajiri, lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Abramu akamwambia Loti, “Tusigombane! Sisi ni jamaa moja. Ebu angalia nchi iliyo mbele yako. Kama ukielekea kushoto nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.” Loti aliitazama nchi yote na kuona kwamba bonde la Mto Yordani lilikuwa zuri sana na lilikuwa na maji tele na nyasi chakula cha wanyama. Kwa hiyo alimwacha Abramu akahamisha mifugo yake kwenye bonde na kukaa karibu na mji wa Sodoma, mji uliokuwa na watu waovu. Naye Abramu akabaki katika Kanaani na Mungu akaahidi kumpa yeye na uzao wake nchi hiyo yote.

Bwana alimtokea Abramu na akamwambia, “Usiogope, mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” Lakini Abrahamu akasema, “Utanipa nini na mimi sina hata mtoto atakayekuwa mrithi wangu?” Naye Mungu akampeleka nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.” Naye Abramu akamwamini BWANA, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

Kisha Mungu akamwambia Abramu kutoa dhabihu maalum ambayo Mungu alimtokea kama mwali wa moto kati ya nusu mbili za mizoga ya wanyama kadhaa na akazungumza naye juu ya wakati ujao.

 

AYA ya KUKUMBUSHA: Warumi 3:21- 24 - Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu, imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia. Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. . .