CBS Stories

Swahili Stories

Yusufu

Mwanzo 37, 39-50

Kupendwa na Baba yake, Kuchukiwa na Ndugu zake

Yakobo aliporudi nchi ya Kanaani alikuwa na wana kumi na wawili. Mzaliwa wa kumi na mmoja, yaani mzaliwa wa kwanza wa Raheli, aliitwa Yusufu. Yakobo alimpenda Yusufu zaidi ya wana wengine. Hasa alimpatia Yusufu koti ya rangi nyingi tofauti maridadi. Wana wengine walipoona kwamba Yakobo alimpenda Yusufu zaidi yao, walimchukia Yusufu. Na pia Yusufu alipowaambia ndoto zake zilizodokeza kwamba siku moja watamsujudia, walizidi kumchukia na kumwonea wivu.

Siku moja, Yusufu alikwenda mahali ambapo ndugu zake walikuwa wakichunga kondoo na mbuzi. Mwanzoni ndugu walipanga kumuua, lakini wakaishia kumuuza kwa wafanyabiashara fulani walipokuwa wakienda Misri. Baadaye walichinja mbuzi na kuifunika kanzu hiyo na damu, kisha wakaipeleka nyumbani kwa Yakobo, ambaye aliomboleza kifo cha Yusufu, akifikiri kwamba mnyama-mwitu amemuua mwana wake.

Watumwa huko Misri

Wakati huo, wafanya biashara walimpeleka Yusufu Misri, wakamuuzia mtu mkuu aliyeitwa Potifa kama mtumwa. Hata ingawa Yusufu alimtumikia Potifa vizuri na alimletea baraka katika nyumba yake, mke wa Potifa alimsingizia kwamba alitaka kumbaka. Kwa hivyo Yusufu alifungwa gerezani.

Alipokuwa gerezani, mfalme wa Misiri, aliyeitwa Farao, aliota ndoto asiyoielewa.

Mfanyakazi wa Farao aliyekuwa amefungwa gerezani pamoja na Yusufu alikumbuka kwamba Yusufu aliweza kutafsiri ndoto. Kwa hivyo Farao alimwita Yusufu. Kwa usaidizi wa Mungu, Yusufu alitafsiri maana ya ndoto. Kungekuwa na miaka saba ya mavuno tele na miaka saba ya njaa kuu. Farao alifurahi sana kwamba Yusufu aliweza kumwambia maana ya ndoto. Kwa hivyo alimfanya mtawala juu ya Misiri. Yusufu alikuwa chini ya Farao tu. Punde, Yusufu alianza kuweka nafaka katika maghala ili kujiandaa kwa njaa. Baada ya miaka saba ya kushiba, kulikuwa na njaa kuu ndani ya Misiri.

Kuungana Tena na Ndugu Zake

Wakati huo, pia kulikuwa na njaa nchi ya Kanaani walipoishi Yakobo na wanake.

Lakini, kwa sababu ya mpango wa Yusufu, bado kulikuwa na nafaka Misiri. Yakobo aliposkia kwamba kulikuwa na nafaka Misri, aliwatuma wanake kumi ili kuenda kuleta chakula. Ndugu za Yusufu walipofika Misri, Yusufu aliwatambua, lakini wao hawakumtambua Yusufu. Wao walikuja wakiinama mbele ya Yusufu kwa sababu alikuwa mkubwa wa Misri. Baada ya muda kwa Yusufu kuwajaribu ndugu zake kwa siri kwa njia kadhaa, aliona kwamba walijuta sana kwa kumuuza utumwani. Kisha Yusufu akajidhihirisha kwao kwa machozi. Akasema, "Mimi ni Yusufu, yule mliyemuuza Misri; msiwe na huzuni, wala msijikasirikie nafsi zenu, kwa kuniuza hapa. Kutakuwa na miaka

saba ya njaa. Lakini Mungu alinituma niwatangulie ili kuhifadhi jamaa yangu na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu. Kwa hiyo, si ninyi mlionileta huku, bali Mungu ndiye aliyeniweka kuwa bwana wa nyumba ya Farao na mtawala wa Misri yote.” Baada ya hayo, Yusufu akawatuma watu wamlete baba yake Yakobo, na jamaa wake wote. Yakobo aliishi huko Misri miaka kumi na saba kabla ya kufa kwake na akarudishwa Kanaani kuzikwa.

Baada ya Yakobo kufa, ndugu za Yusufu waliogopa kwamba Yusufu angewaadhibu kwa sababu ya yale waliyomtendea, hivyo walimwomba tena awasamehe. Lakini Yusufu akawaambia, "Msiogope! Je, mimi ni badala ya Mungu? Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia kuwa mema ili kutimiza yale yanayofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. Msiogope, nitawapa riziki ninyi na watoto wenu.” Naye akawatuliza na kusema nao kwa upole.