Samweli alipokuwa mkongwe, Waisraeli walimwambia, “Tunataka mfalme kama mataifa mengine.”
Samweli hakufurahia lakini Mungu akasema, “Waisraeli wananikataa kama Mfalme. Tangu nilipowaondoa Misri, waliasi dhidi yangu na kuiabudu miungu mingine. Kwa hivyo wape wanachotaka. Lakini kwanza, uwaonye watakavyotawaliwa na wafalme.”
Samweli alijaribu kubadilisha mawazo yao na akasema, “Mfalme atalazimisha wana wenu kupigana katika jeshi lake. Na atachukua mashamba yenu mazuri na mifugo yenu iliyo bora. Nanyi mtakuwa watumwa wake.”
Lakini Waisraeli hawakumsikiza Samweli wakasema, “La! Tunataka mfalme kama mataifa mengine, yaani mfalme anayeweza kutuongoza katika vita.”
Basi Mungu alimwongoza Samweli kwenye kijana aliyeitwa Sauli. Samueli alimtia mafuta kumweka wakfu akisema, “Bwana anakutia mafuta wewe kama mfalme wa watu wake wa Israeli.”
Kisha Samweli akamleta Sauli mbele ya watu, nao wakashangilia wakisema “Mfalme aishi muda mrefu.”
Sauli aliwasaidia Waisraeli kushinda maadui wao, lakini alianza kujitegemea badala ya kufuata Mungu. Siku moja, badala ya kumgojea kuhani wa Mungu Samueli amtolee Mungu dhabihu kabla ya vita, aliwaogopa maadui na akamtolea Mungu dhabihu yeye mwenyewe hata ingawa yeye hakuwa kuhani. Mungu akakasirika sana.
Wakati mwingine Mungu akaongea kupitia kwa Samweli na kumwambia avamie Waameleki kulipiza kisasi kwa sababu Waameliki walikuwa wakiwaavamia Waisraeli waliporudi kutoka Misri. Waameleki waliabudu sanamu. Mungu akasema, “Mharibu kila kitu hata mifugo.” Lakini Sauli hakumwua mfalme wao au wanyama wazuri. Pia Sauli alijisimamishia sanamu ya ukumbusho.
Baada ya vita, Samueli akamwendea Sauli. Naye Sauli akamwambia, “Bwana akubariki! Nilifanya kile Mungu aliniambia wakati huu.”.
Samweli akasema, “Ni kweli? Maana yake nini basi hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu na huu mlio wa ng’ombe ninaousikia?”
Sauli akamjibu, “Majeshi waliweka wanyama walio bora zaidi kwa kutoa kama dhabihu kwa Bwana Mungu wako. Lakini tuliharibu kila kitu kingine chochote! Tulimtii Mungu!”
“Nyamaza!” aliamuru Samweli. “Je, unafikiri Bwana anapenda dhabihu zaidi ya utiifu? Kutii ni bora kuliko sadaka. Uasi na kiburi ni mbaya kama ibada ya sanamu. Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, yeye amekukataa wewe kuwa mfalme." Samweli akageuka ili aondoke, lakini Sauli akalishika vazi lake, nalo likararua jirani."
Hatimaye Sauli akasema, “Sawa, nimefanya dhambi. Nilikiuka agizo la Mungu.
Niliogopa watu na hivyo nikakubali. Sasa nakuomba, unisamehe dhambi yangu, urudi pamoja nami, ukaniheshimu mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli; urudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu BWANA.” Hivyo Samweli akarudi, naye Sauli akamwabudu Bwana, lakini Samweli akamwua mfalme wa Waameleki mbele ya Bwana. Kisha akaenda na hakumwona Sauli tena akamwombolezea.