Mwanzo
Hapo mwanzo wa vitu vyote, Mungu alipoziumba mbingu na dunia, dunia haikuwa na umbo na ilikuwa tupu pia. Giza lilifunika vilindi vya maji. Roho wa Mungu alitulia juu ya maji.
Siku Sita za Uumbaji
Mungu akasema, “Iwe nuru,” Ikawa nuru. Mungu akatenga nuru na giza. Akaita nuru “mchana,” na giza “usiku.” Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya kwanza.
Mungu akasema, “Iwe anga katikati ya maji kuyatenga maji yaliyo juu ya anga kutoka maji yaliyo chini ya anga.” Ikawa hivyo. Mungu akaliita hilo anga “mbingu.” Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya pili.
Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike mahali pamoja, ili inchi kavu ionekane.” Ikawa hivyo. Mungu akaiita ardhi “nchi”; na akayaita makusanyiko ya maji “bahari”; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, “Nchi ifunikwe kwa miti mizuri yote na kila aina ya mmea wa kijani uliokuwa mzuri kwa chakula.” Mungu akaibariki ili ingezidi kuzaana kulingana na aina yao. Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya tatu.
Mungu akasema, “Mbingu ijazwe kwa mianga yote mbalimbali – mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku, na nyota zote.” Huo mwanga mkubwa ulikuwa jua, na mdogo ulikuwa mwezi. Akaumba nyota. Akasema, “Mianga iwe ishara za siku na misimu na matukio.” Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya nne.
Mungu akasema, “Mbingu ijazwe kwa viumbe vinavyopaa vyote na mabahari yajazwe kwa viumbe vinavyoogelea.” Mungu akavibariki ili vingezidi kuzaana kulingana na aina yao. Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya tano.
Mungu akasema, “Nchi ijazwe kwa wanyama, wanyama wa mwituni, wanyama wa kufuga na wanaotambaa.” Mungu akawabariki ili wangezidi kuzaana kulingana na aina yao. Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Katika Mfano wa Mungu
Mungu akasema, “Tuumbe mtu katika sura na mfano wetu. Tutamwumba wa kiume na wa kike na tutawapa mamlaka juu ya uumbaji wote.” Kwa hivyo Mungu alifanya hivyo. Mungu akawabariki ili wangezidi kuzaana na wajaze dunia. Mungu akawapa kila mmea wa kijani kwa chakula. Na Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na kilikuwa chema sana. Jioni ikapita asubuhi ikaja, kwa hivyo siku ya sita.
Pumziko la Mungu
Kwa siku ya saba, Mungu alikuwa amemaliza kazi yake yote ya uumbaji. Kwa hivyo alipumzika. Hii ndiyo sababu Mungu alitenga siku ya saba kwa sababu hii ndiyo siku alipumzika baada ya uumbaji.
Hapo mwanzo wa vitu vyote, Mungu alipoziumba mbingu na dunia, dunia haikuwa na umbo na ilikuwa tupu pia. Giza lilifunika vilindi vya maji. Roho wa Mungu alitulia juu ya maji.
Mungu akasema, “Iwe nuru,” Ikawa nuru. Mungu akatenga nuru na giza. Akaita nuru “Mchana,” na giza “Usiku.” Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ilikuwa siku ya kwanza.
Siku ya pili, aliumba anga kwa kugawanya maji yaliyo juu na maji yaliyo chini.
Siku ya tatu, aligawanya bahari na nchi kavu na akaumba mimea na miti yote mizuri kwa chakula.
Siku ya nne, aliumba mianga angani - jua litawale mchana, mwezi utawale usiku, na nyota. Alizifanya kuwa ishara kwa siku, majira na matukio.
Siku ya tano akafanya ndege na samaki.
Siku ya sita, alifanya mambo makubwa mawili. Kwanza aliumba wanyama wote wanaotembea ardhini. Na kila wakati alipoumba kiumbe hai - mmea, ndege, samaki, au mnyama - alikbariki kuwa na uwezo wa kuzaana kulingana na aina yake. Na karibu kila siku alipomaliza kuunba kitu alisema, "Ni nzuri."
Kisha, pia katika siku ya sita, Mungu akasema, “Tuumbe mtu katika sura na mfano wetu.” “Tumwumbe wa kiume na wa kike na tuwape mamlaka juu ya uumbaji wote.” Kwa hivyo Mungu alifanya hivyo. Mungu akawabariki ili wazidi kuzaana na wajaze dunia.
Mungu akawapa kila mmea wa kijani kwa chakula. Na Mungu akaona ya kuwa ni nzuri sana. Hiyo ilikuwa siku ya sita.
Kwa siku ya saba, Mungu alikuwa amemaliza kazi yake yote ya uumbaji. Kwa hivyo alipumzika. Hii ndiyo sababu Mungu alitenga siku ya saba kwa sababu hii ndiyo siku alipumzika baada ya uumbaji.