CBS Stories

Swahili Stories

Pasaka

Kutoka 12

Ugumu wa Moyo wa Farao / Pigo Moja la Mwisho

Baada ya mapigo tisa ya kwanza, Mungu alimwambia Musa, “Nimefanya moyo wa Farao kuwa mgumu kuwaadhibu WaMisri kwa miungu yao. Ninafanya ishara hizi ili mtawambia watoto wenu na wajukuu wenu hata mjue kwamba mimi ndimi Bwana!

Nitalileta pigo lingine moja kwa Misri halafu Farao atawafukuza kabisa.

Maelekezo ya Mungu

Haya ndio yalikuwa maelekezo ya Mungu kwa Waisraeli.

Mnisikilize kwa makini.

  1. “Lazima kila familia (au familia mbili pamoja kama ni familia ndogo) kuchukua mwana kondoo au mbuzi moja wa mwaka mmoja wa kiume asiye na waa achinjwe jioni giza linapoingia.
  2. “Chovya mti unaitwa hisopo katika damu na mpake pande zote mbili za mlango wa nyumba na juu ya mlango, katika ile nyumba ambamo mtamla mwana kondoo. Kisha kaeni ndani ya nyumba na ishara ya damu mpaka asubuhi.
  3. “Mwichome nyama na kuila Msiyaache mabaki hata msivunje mifupa. Mle na mboga chungu na mkate bila chachu. Mle haraka mkivaa mavazi ya safari.”

“Usiku ule nitapita katikati ya Misri na kuwauwa kila mzaliwa wa kwanza kuwaadhibu Wamisri kwa kuwaabudu miungu ya uongo. Lakini damu itakuwa ishara kwenu. Nitakapoiona damu juu ya mlango nitapita juu yenu.

“Ni lazima msherehekee sherehe hii kila mwaka. Watoto wenu watakapowaulizeni, ‘Maana ya sherehe ni nini?’ Waambieni, ‘Kwa siku hiyo, Bwana alituleta kutoka utumwa katika Misri.’”

Kutoa Mwanakondoo / Ukombozi

Basi, watu walitoa dhabihu ya wanyama na damu ikamwagwa kisha wakaiweka kwenye milango. Usiku wa manane Mungu alipita kwenye Misri, akawaua kila mzaliwa wa kwanza – kutoka jumba la ufalme la Farao, mpaka mfungwa gerezani na wazaliwa wa kwanza wa wanyama pia. Lakini Mungu alipoiona damu ya dhabihu ya mwana kondoo kamilifu kwenye milango ya Waisraeli, alipita juu yao. Kulikuwa kimya kule Waisraeli walikuwa, hata mbwa hawakubweka. Lakini mahali Wamisri walipoishi, kulikuwa na kilio kikuu katika usiku.

Usiku, bado kukiwa na giza Farao aliwaita Musa na Haruni akasema, “Chukueni kila kitu mlicho nacho mwondoke!” Na majirani wao wa Wamisri walisema, “Ndiyo nendeni au tutakufa!” Nao wakawapa Waisraeli vitu vyao vya thamani kama dhahabu, fedha na kadhalika, kama vile Mungu alivyowaambia Musa, hata Abrahamu zamani.

Siku hiyo Mungu aliwakomboa watu wake kutoka nchi ya Misri. Walikuwa karibu wanaume laki sita na wanawake, watoto na mifugo yao.