CBS Stories

Swahili Stories

Nikodemo

Yohana 3:1-21

Hii ni hadithi ya Nikodemo.

Siku moja Yesu alikuwa katika Yerusalemu karibu na wakati wa Pasaka na alikuwa amefunza siku nzima. Ilipofika jioni, alirudi pahali ambapo alikaa.  Giza ilipoingia, mtu fulani alikuja kumwona.  Jina lake Nikodemo. Alikuwa mojawapo wa vinogozi wa Wayahudi.

Nikodemo akasema, “Rabii, tunajua kwamba umetoka kwa Mungu, kwa maana hakuna awezaye kufanya mambo unayofanya Mungu asipokuwa naye.”

Yesu akmjibu, “Nakuambia, ukweli, usipozaliwa mara ya pili, huwezi kuona uflame wa Mungu.”

Sasa nikodemo alichanganyikiwa. Akasema, “Mtu anawezaje kuzaliwa tena anapokuwa mzee?  Anaweza kuingia tena katika tumbo ya mamake mara ya pili na kutoka tena?”  Yesu akajibu “Amin amin, nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa roho ni roho. Lazima uzaliwe mara ya pili.

Nikodemo akiwa bado amechanganyikiwa akamwuliza, “Haya yanawezekanaje?”

Kisha Yesu akamsimulia hadithi. “Je, unakumbuka hadithi ya Musa akiwaongoza Waisraeli jangwani? Waisraeli walikosa kumtii Mungu naye akawatuma nyoka wengi kwenye kambi. Waliwauma watu wengi na kuuma kwao kulikuwa kama moto. Wengi wakawa wagonjwa na hata wengine walikufa. Kisha Israeli wakamlilia Mungu, “Tusaidie!” Naye Mungu akamwambia Musa ni lipi wangefanya. Akasema, “Mtengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti.  Kisha uweke mti huo katikati ya kampi. Mtu yeyote atakayeumwa na nyoka, atapaswa kuangalia nyoka wa shaba, naye hatakufa.”

Kisha Yesu akamwambia Nikodemo, “Kama vile Musa alimwinua yule nyoka jangwani, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoinuliwa ili yeyote amwaminiye aweze kupata uzima wa milele. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa Mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.”

“Yeye amwaminiye hahukumiwi bali alisiye mwamini amehukumiwa tayari kwa sababu hajaamini katika jina la Mwana wa Mungu wa pekee. Huu ndio uamuzi; Nuru imekuja ulimwenguni, lakini watu wamependa giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu.”

Huu ndio mwisho wa hadithi.