Ahadi za Mungu kwa Watu Wake wa Agano
Miezi miwili baada ya Waisraeli kutoka Misri, walitua mbele ya Mlima wa Sinai. Musa alipanda mlimani kukutana na Mungu. Mungu akasema, “Waambie watoto wa Israeli, ‘Mmeona jinsi niliwaokoa kutoka Misri. Mkinitii kikamilifu na kutimiza ahadi yangu, ndipo kutoka kwa mataifa yote, mtakuwa urithi wangu wa thamani. Mtakuwa ufalme wa makuhani na taifa takatifu”
Musa alipowaambia watu, wakasema, Tutafanya kila kitu Bwana alichosema.”
Utakaso na Nguvu
Ndipo Mungu akasema, “Musa, nitakujia katika wingu ili watu wote wataniskia nikiongea nawe na watakuamini. Waambie watu kujitakasa kwa siku mbili nami nitakuja siku ya tatu. Usiruhusu mtu yeyote au mnyama kuuguza mlima. Wakifanya hivyo watakufa kwa maana hapa ni pahali patakatifu.” Watu walimtii Mungu na siku ya tatu wingu zito likafunika mlima. Kulikuwa na radi na umeme na kelele kuu kama sauti ya tarumbeta. Moshi ulichemka kutoka kwa mlima kama unaotoka katika tanuru na mlima wote ukatetemeka. Waisraeli wote walitetemeka kwa hofu kuu.
Amri Kumi
Baadaye Musa akapanda juu mlimani na Mungu akampa amri kumi:
Pia Mungu, aliwapa sheria nyingine nyingi ambazo zilitungwa hasa ili kuwasaidia Waisraeli wafanye kazi kama taifa chini ya Mungu.
Majibu ya Wananchi
Baada ya hayo yote, watu walikuwa wakitetemeka kwa hofu. Musa akawaambia, “Msiogope. Mungu amekuja kuwajaribu, ili hofu yake iwe pamoja nanyi ili kuwaepusha na dhambi anapowaongoza katika nchi ya ahadi. Mtakapofika huko, msifanye agano na
Wakanaani au miungu yao, wala kuishi pamoja nao, kwa sababu watawafanya mtende dhambi dhidi yangu.”
Asubuhi iliyofuata Musa alijenga madhabahu chini ya mlima na kutoa dhabihu kwa Mungu ili damu ikamwagike. Kisha Musa na msaidizi wake, Yoshua, wakapanda tena mlimani na Mungu akampa Musa nakala zingine mbili za agano kati yake na Israeli, zilizoandikwa katika mawe. Wingu liliufunika mlima na kila watu walipotazama juu, waliona utukufu wa Mungu uking'aa kama moto juu yao.