CBS Stories

Swahili Stories

Manabii wanatabiri kuja kwa Mwokozi Aliyeahidiwa na Agano Jipya

Manabii walionya watu wa Mungu kuhusu hukumu kwa dhambi zao, lakini pia waliwaambia kuhusu huruma na msamaha wa Mungu kwa watu waliotubu na kumwamini. Waliwakumbusha kuhusu Mwokozi ambaye Mungu aliyekuwa amehidi zamani. Walisema, “Kuna Mmoja ambaye anakuja kuwaokoa kutoka kwenye dhambi zenu.”

Nabii Isaya alisema kwa Wayahudi, “Bwana mwenyewe atakupa ishara: bikira atamzaa mwana. Atamwita Immanueli, maana yake ‘Mungu pamoja nasi.’ Ataitwa Mfalme wa Amani. Enzi yake haitakuwa na mwisho kamwe.” Pia alitabiri kuhusu Mwokozi huyu kama mtumishi, kwamba atateseka na kudharauliwa, ambaye ataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini manabii walitabiri kwamba Mwokozi atafufuka. Na pia walitabiri vitu vinginevyo ambavyo vitamfanyikia Mwokozi. Kwa mfano, Mikono na miguu kudungika, kuuzwa kwa shilingi thelathini, kusalitiwa na rafiki, kuhesabiwa pamoja na wenye dhambi, n.k.

Manabii waliongea kuhusu Agano Jipya ambalo lingetimilia katika Mwokozi aliyeahidiwa. Mungu alisema kupitia nabii Yeremia, “Watu wangu walivunja agano langu lakini nitafanya agano jipya nao. Nitawatoa katika utumwa. Nitaweka sheria yangu katika akili zao na kuiandika kwa mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao na watakuwa watu wangu.”

Mungu alimwambia nabii Ezekieli pia kitu kama hicho akisema, “Nitawapatia moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitaondoa kutoka kwenu moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama . Nitaweka Roho wangu ndani yenu na kuwafanya kufuata maagizo yangu na kuwa waangalifu kutii amri zangu.

Baada ya watu wa Mungu kurudi Yerusalemu kutoka utumwani Babiloni, na baada ya kujenga Yerusalemu na hekalu, Mungu alisimama kuongea kupitia manabii kwa miaka mia nne. Lakini katika wakati huo wa mateso, bado Wayahudi wengine walikumbuka ahadi za Mungu kuwaletea Mwokozi.

 

Baadhi ya Unabii wa Agano la Kale kuhusu Mwokozi Ambaye Angekuja

Ushairi wa Ahadi

Unabii

Ushairi wa Kutimiza

Isaya    9:7

Atarithi kiti cha enzi cha daudi

Mathayo 1:1

Mika 5:2

Pahali pa kuzaliwa kwake

Mathayo 2:1

Danieli     9:25

Mzaliwa atakapozaliwa

Luka 2:1-2

Isaya    7:14

Nani atakayemzaa

Mathayo 1:18

Yeremiah 31:15

Watoto wengi watauwawa

Mathayo 2:16

Hosea 11:1

Kutoroka kwake hadi Misri

Mathayo 2:14

Isaya 9:1-2

Kazi yake katika Galilaya

Mathayo 4:12-16

Zaburi 110:4

Yeye ni kuhani kama Melkizedeki

Waebrania 6:20

Isaya 53:3

Atakataliwa na Waisraeli

Yohana 1:11

Isaya 11:2

Baadhi ya tabia zake

Luka 2:52

Zakaria 9:9

Anakuja katika Yerusalemu

Mathayo 21:1-11

Zaburi 41:9

Alisalitiwa na rafiki

Marko 14:10

Zakaria 11:12-13

Vipande thelathini vya fedha vililipwa

Mathayo 26:15

Zaburi 27:12

Mashahidi wa uwongo walimshtaki

Mathayo 26:59-62

Isaya 53:7

Alinyamaza aliposhtakiwa

Mathayo 26:62-63

Isaya 50:6

Alipigwa na kutemewa mate

Marko 14:65

Zaburi 69:4

Alichukiwa bila sababu

Yohana 15:23-25

Isaya 53:4-5

Aliumia kwa ajili ya wengine

Mathayo 8:16-17

Isaya 53:12

Alisulubishwa kati ya wenye dhambi

Mathayo 27:38

Zaburi 22:16 &

Zakaria 12:10

Mikono yake na miguu ilidungwa

Yohana 20:25-27 &

Yohana 19:37

Zaburi 22:6-8

Alithihakiwa na kutukanwa

Mathayo 27:39-44

Zaburi 69:21

Alipewa siki kunywa

Yohana 19:29

Isaya 53:12

Anawaombea maadui wake

Luka 24:34

Zaburi 22:18

Walilichezea kamari vazi lake

Marko 15:24

Zaburi 16:10

Anafufuka kutoka kwenye wafu

Luka 24:1-8

Zaburi 68:18

Anapaa Mbinguni

Luka 24:50-51

Mwanzo 12:3

Kupitia kwake makuja Baraka aliyoahidiwa Abrahamu

Wagalatia 3:14-29