Kulikuwa na mwanamume aliyeitwa Lazaro aliyekuwa rafiki wa karibu wa Yesu. Alikuwa na dada wawili walioitwa Mariamu na Martha. Siku moja, Lazaro alikuwa mgonjwa sana na dada zake walimtumia Yesu ujumbe. “Bwana, umpendaye ni mgonjwa sana.” Yesu alipoupokea ujumbe aliwaambia wanafunzi wake, “Ungonjwa huu hautaleta kifo lakini utukufu wa Mungu.”
Yesu alimpenda Lazaro na dada zake wawili, lakini alikaa siku mbili zaidi pahali hapo kabla ya kusafiri na wanafunzi wake nyumbani kwa Lazaro. Aliwaambia wanafunzi wake, “Lazaro amekufa, na kwa ajili yenu nina furaha kwa sababu sikuwepo, ili mweze kuamini. Lakini ebu twende kwao.”Alipofika, Lazaro alikuwa amekufa siku nne zilizopita . Alipokaribia nyumbani kwao alipata watu wengi wakilia na kuomboleza Lazaro. Martha akamjia Yesu na kusema, “Bwana, ungekuwa hapa tu, kaka wangu hangekufa. Lakini ninajua kwamba, yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.”
Yesu akamwambia, “Lazaro atafufuka”.
Martha akasema, “Ndiyo ninajua kwamba, atafufuka tena siku ya mwisho”.
Lakini Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uzima. Yeyote anayeniamini ataishi hata ikiwa atakufa. “Je, unayaamini haya?”
Martha alisema, “Ndiyo ninaamini, wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.” Kisha Martha alikimbia kwake Maria na kumwambia kwamba, “Yesu yuko hapa.”
Maria alipokuja kwake Yesu, alisema, “ikiwa ungekuwa hapa, kaka wangu hangekufa.”
Kisha Yesu alikuja kwenye kaburi la Lazaro, na akalia. Yesu akasema, “Liondoeni jiwe kutoka kwa kaburi.”
Martha akasema, “Lakini amekufa zapita siku nne. Sasa kutakuwa na harufu mbaya sana!”
Kisha Yesu akasema, ikiwa utaamini utaona utukufu wa Mungu.” Walipoliondoa jiwe, Yesu aliomba, “Baba, asante sana kwa sababu umenisikia ili watu hawa waweze kuamini kwamba umenituma.” Kisha aliamuru, “Lazaro, toka nje!” Naye Lazaro akatoka kwenye kaburi na Yesu akasema, “Ziondoeni sanda na mwaache aende.” Watu wengi walimwamini siku hiyo. Huu ndio mwisho wa hadithi.