CBS Stories

Swahili Stories

Kuzaliwa na Kutoroka kwa Musa

Kutoka 1-2

Yusufu aliaga dunia na akazikwa huko Misri. Na familia ya Yakobo wakawa watu wengi. Waliitwa watu wa Israeli au Waebrania. Basi kukawa na mfalme mpya katika Misri asiyemjua Yusufu. Alipoona kwamba watu wa Israeli walikuwa wengi sana, aliogopa, akawafanya watumwa. Aliogopa kwamba wangewashambulia Wamisri na kuwashinda, hivyo hata akaamuru kwamba kila mtoto wa kiume aliyezaliwa katika Israeli auawe anapozaliwa. Lakini wakunga Waisraeli walimheshimu Mungu na hawakufanya walivyoambiwa na Farao. Bali Mungu aliwalinda kutoka na Farao. Basi Waisraeli wakaendelea kuongezeka.

Palikuwa na familia ya Israeli kutoka ukoo wa Lawi nao wakawa na mtoto wa kiume aliyekuwa mrembo. Walimficha kwa muda wa miezi mitatu, lakini hatimaye wakamweka katika kikapu kilichofunikwa kwa lami na kukiacha kikielea mtoni. Dada mkubwa wa mtoto huyo aliitwa Miriamu. Alikaa kwenye karibu na kikapu akitazama ni kitu kipi kingemfanyikia mtoto huyo.

Basi binti wa mfalme wa Misri alikuja kwenye mto Nile pamoja na marafiki wake, akamwona mtoto akamchukua awe mwana wake. Akamwita jina lake Musa kwa maana alimtoa kwenye maji. Miriamu akamjia binti wa mfalme na kumwuliza, “Je ungependa nikutafutie mwanamke Mwebrania kukunyonyeshea mtoto huyu?”

Binti wa mfalme akasema, “Ndiyo, nitafutie mwanamke nami nitamlipa kumnyonyesha mtoto huyu.” Ikawa hivyo. Mtoto huyu alipokuwa mkubwa, Mama yake alimpelekea binti wa mfalme naye akawa mwana wake. Basi Musa akakulia katika jumba la mfalme wa Misri.

Wakati Musa alipokuwa mtu mzima, siku moja alitoka kati ya watu wake Waisraeli. Hapo aliona Mmisri akimpiga Mwisraeli. Aliangalia pande zote asione mtu yeyote, kisha akamwua Mmisri huyo na kuuficha mwili wake. Lakini jambo hili lilijulikana naye Musa akatorokea jangwani.

Lakini Mungu aliyaona mateso ya watu wake Waisraeli, akakumbuka agano lake na Abrahamu, Isaka, na Yakobo.