CBS Stories

Swahili Stories

Kusulubiwa

Jn. 19:16b-42; Mat. 27:27-61; Mk. 15:16-47; Lk. 23:26-56

Hii ni hadithi ya kusulubishwa kwa Yesu.

Sasa Yesu alikuwa amepigwa vibaya, na maaskari walikuwa wameweka kofia ya miiba kwenye kichwa chake kumdhihaki.  Damu ilitiririka kwenye uso wake na kwenye mgongo wake alipokuwa amepigwa. Baada ya Pilato kuwapa maaskari Yesu kusulubishwa, Maaskari wa Kirumi walimfanya Yesu kubeba msalaba wake mwenyewe. Yesu alipoubeba mpaka pahali alipoweza, maaskari wakalazimisha mtu kutoka kusanyiko (kundi) kumbebea Yesu msalaba. Jina lake lilikuwa Simoni Mkurene. Wakatembea kupitia barabara za Yerusalemu na nje ya mji na hadi juu ya mlima ulioitwa Golgotha.

Walipofika Golgotha, walimsulubisha Yesu pamoja na wezi wawili. Kwanza maaskari waliweka mbao chini kama msalaba na wakamweka Yesu juu ya hizo mbao. Halafu wakaifungia mikono yake kwa mbao kwa kutumia kamba na wakagonga misumari mikubwa kupitia mikono na miguu yake hadi kwenye mbao. Hivi ndivyo walivyoweka Yesu msalabani. Halafu, kwa kutumia kamba, waliuinua msalaba hewani wakausimamisha. Pia wakawasulubisha wezi wawili vivyo hivyo, mmoja kwa kila upande wa Yesu.  Halafu wakaketi chini ya msalaba wakaanza kuipigia kura nguo yake.

Kulikuwa na watu wengi karibu wakitazama kuona ni nini kingefanyika. Kulikuwa na wanawake waliomfuata katika huduma yake yote. Walikuwa wanasimama wakitazama kila kitu kwa karibu. Makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuweko pia. Walikuwa wakimdhihaki na kumtusi na kumchekelea. “Aliwaokoa wengine. Kwa nini hawezi kujiokoa?”

Mmoja wa wezi pia alimdhihaki na kumtukana Yesu. Lakini mwingine alimkemea akisema, “Hapana! Nyamaza!  Sisi tuna hatia. Tunastahili kusulubishwa, bali mtu huyu hana hatia.” Kisha akamwambia Yesu, “Nikumbuke utakapofika katika ufalme wako.” Yesu akamjibu, “Nakuambia ukweli, leo hii, utakuwa nami katika Paradiso.”

Sasa ilipokuwa karibu na adhuhuri kulikuwa na giza kuu katika nchi yote mpaka saa tisa. Wakati huo kulikuwa na tetemeko la ardhi kubwa sana na watu wote waliogopa. Wakati huo, Yesu alilia kwa sauti kuu, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”  Pia akasema, “Imeisha!”  Na akatoa roho kwa Mungu akafa. Hata pazia ndani ya hekalu iliraruka katika vipande viwili toka juu hadi chini. Kulikuwa na amrijeshi wa Kirumi chini ya msalaba, alipoona mambo haya yote, akasema, “Hakika, huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

Ilikuwa mila ya Wayahudi kutoacha maiti zikining’inia usiku wote hata siku ya Sabato. Kwa hivyo, wakawaomba maaskari kumaliza kazi yao. Maaskari walivunja miguu ya wezi wawili nao walikufa haraka. Lakini walipomwendea Yesu, walipata kwamba alikuwa ameshakufa.  Kwa hivyo hawakuivunja miguu yake kama ilivyotabiriwa.  Mmoja wa maaskari alimdunga mkuki kwenye upande wa Yesu. Alipotoa mkuki, damu na maji yalimwagika kutoka mwili wa Yesu.

Mwanamume aliyeitwa Yusufu wa Arimathea aliomba ruhusa kuchukua mwili wa Yesu. Akachukua mwili na kuuzika katika kaburi iliyokuwa karibu ambalo halikuwa limetumika kamwe. Na akabingirisha jiwe juu ya kaburi na akaenda zake. Lakini wanawake waliomfuata Yesu katika huduma yake yote walitazama mambo yote kwa uangalifu na kuona pahali ambapo Yusufu alimzika Yesu.

Huu ndio mwisho wa hadithi.