Yohana alikuwa mwana wa mkuhani aliyeitwa Zechariah. Malaika wa Mungu alimwambia Zechariah kwamba mwana wake angekuwa na roho ya Elia na angewasaidia watu kutayarisha mioyo yao kupokea Mwokozi aliyeahidiwa. Yohana alipokua akawa mwanamume, Alijionyesha kwa Israeli. Alihubiri jangwani, “Tubuni! Kwa maana ufalme wa Mungu uko karibu!” Na wale waliotubu walibatizwa katika mto wa Yordani.
Na sasa makundi makubwa yalikuwa yakienda kumsikia akiongea na pia kubatizwa. Lakini Makuhani wakuu na walimu wa sheria, yaani viongozi wa Israeli, walibaki katika Yerusalemu na kuwatuma wajumbe wao kwa Yohana. Wajumbe hao waliuliza, “Wewe ndiwe Kristo?” Yohana alisema, “Mimi siye.” Waliuliza, “Wewe ni Eliya?” Yohana alisema, “La.” “Basi wewe ni nani?” Yohana alisema, “Mimi ni sauti ya mutu aliae nyikani, ‘Tayarisheni njia ya Bwana.” Kuna yule ajaye baada yangu, ambaye ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu alikuweko kabla ya mimi.”
Wakati huo, Yesu pia alikuja ili naye abatizwe na Yohana. Alipokuja juu kutoka majini, Roho Mtakatifu alimshukia nazo mbingu zikafunguka na sauti ikatoka juu mbinguni ikisema, “Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.”
Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akitembea katikati ya makutano na akasema, “Tazameni! Mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye nilikuwa nikiwambieni nilposema, “Kuna mmoja ajaye baada yangu, ambaye ni mkuu kuniliko mimi kwa sababu alikuweko kabla yangu!”
Na huu ndio mwisho wa hadithi.