Yesu alizikwa kabla ya jua kutua siku ya Ijumaa, naye Pilato akawaweka maaskari wanne wa Kirumi kulinda kaburi. Sabato ilimalizika jioni ya Jumamosi. Kabla ya jua kuchomoza jumapili asubuhi, wanawake walienda kwenye kaburi wakiwa na manukato na mafuta kuutayarisha mwili wa Yesu. Wakiwa njiani waliulizana, “Ni nani atakayetuondolea jiwe?” Kisha kukawa na mtetemeko mwingine mkubwa. Malaika wa Bwana alilimbingirisha jiwe na kulikalia! Maasakari wa Kirumi waliogopa sana wakaanguka chini kama waliokufa.
Malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua mnamtafuta Yesu, lakini hayuko hapa. Amefufuka kama vile alivyosema. Je, hamkumbuki aliyosema – ‘Mwana wa Adamu atapeanwa katika mikono ya wenye dhambi, asulubishwe na baada ya siku tatu baadaye afufuke’? Halafu malaika akasema, “Njooni mtazame alipolazwa. Nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake anaenda Galilaya mbele yenu na mtamwona huko. Sasa msisahau yale niliyowaambia.” Nao wanawake hao wakakimbia kwenda kutafuta wanafunzi wa Yesu.
Wanawake walipoondoka, baadhi ya maaskari walinzi kwenye kaburi walienda kwa makunani wakuu na kuwaambia kilichotendeka. Hao viongozi wa dini wakawapa hao maaskari pesa nyingi wakisema, “Lazima mseme kwamba wanafunzi wake walikuja na kuiba mwili tulipokuwa tumelala.”
Wanawake walipowapata wanafunzi waliwaambia kila kitu kilichofanyika. Lakini wengi wa wanafunzi hawakuwaamini lakini Petro na Yohana walikimbia kwenye kaburi. Yohana akafika kaburini kwanza kwa kuwa alikimbia haraka akaangalia ndani lakini hakuingia. Petro alipofika aliingia moja kwa moja ndani ya kaburi. Aliona sanda ambazo Yesu alikuwa amefungwa. Lakini hapakuwa na mwili ndani ya sanda! Kisha Yohana akaingia ndani pia. Wote wakaona kwamba kaburi lilikuwa tupu bila mwili.
Walirudia wanafunzi wengine mahali walipokuwa na wakawaambia walivyoona. Wote walistaajabu kwamba Yesu alikuwa amefufuka. Jioni ya siku hiyo Yesu alitokea katikati ya wanafunzi walipokuwa wamejificha, lakini Tomaso hakuwepo. Baadaye walipomwambia Tomaso kuhusu kujitokeza kwa Yesu, alijibu, “Sitaamini hadi nione alama za misumari na kuweka kidole ubavuni.”
Baadaye wanafunzi walipokuwa katika chumba cha juu na mlango umefungwa, Yesu aliwatokea. Akasema, “Amani iwe kwenu. Tomaso, njoo, uone mikono yangu na uweke kidole ubavuni mwangu. Niamini mimi!” Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” Yesu akajibu, “Umeona ukaamini lakini wamebarikiwa wale wanaoamini bila kuona.”
Huu ndio mwisho wa hadithi.