Siku hiyo hiyo, wawili kati ya wafuasi wa Yesu wakawa wanaenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau umbali wa kilomita saba au kumi kutoka Yerusalem. Wakawa wakizungumza juu ya yale yaliyo tukia wakati huo. Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea akatembea pamoja nao. Walimwona kwa macho lakini hawakumtambua.
Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza mnapotembea??” Nao wakisimama kimya, nyuzo zao zikiwa zimejikunja kwa huzuni. Mmoja wao aitwaye Kleopa, akamjibu “Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliotukia huko siku hizi?”
Naye akawauliza “Mambo gani?”
Wao wakamjibu, “Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote, makuani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa wakamsulubisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli.”
“Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yalipotendeka tena wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushtua walipokwenda kaburini mapema asubuhi wasikute mwili wake. Wakarudi wakasema ya kwamba walitokewa na malaika waliowaambia kwamba yu hai. Wengine wetu walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo, kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.”
Kisha msafiri (yaani Yesu) akawaambia, “Enyi msiofahamu wenye mioyo mizito kuamini yote yaliyosemwa na manabii. Je, haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake”? Akaanza kuwafunulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika maandiko matakatifu kuanzia Musa hadi manabii wote.
Walipokikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu alifanya kama anataka kuendelea mbele lakini wao wakamsihi wakisema, “Kaa pamoja nasi kwa kuwa kumekuchwa na usiku unakaribia.” Basi akaingia kijijini akakaa pamoja nao.
Walipokaa kula Yesu akachukua mkate akaubariki, akaumega, akawapa. Mara macho yao yakafumbuliwa wakamtambua. Kisha akatoweka mbele yao. Basi wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa akitufafanulia maandiko matakatifu kule njiani?”
Wakaondoka saa ile ile wakarudi Yerusalemu, wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao wamekusanyika, wakasema, “Hakika Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simioni.”
Basi nao wale wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.
Huu nido mwisho wa hadithi.