Maelezo ya Maskani
Baada ya wana Waisraeli kutubu kwa kumwabudu ndama wa dhahabu, ilikuwa wakati wa kujenga maskani, yaani pahali pa Mungu kuishi nao. Watu walizileta sadaka za vitu vyote vya thamani ambavyo wafanya kazi wangetumia kwa kujenga. Ilichikua mwaka mmoja kujenga maskani kama Mungu alivyomwambia Musa .
Maskani ilipokwisha kujengwa, ilikuwa kama hema kubwa iliyogawanywa kwa pazia nzito. Katika chumba cha mbele ya pazia, yaani pahali patakatifu, mlikuwa na vitu vitatu:
Katika chumba nyuma ya pazia, yaani pahali patakatifa zaidi, kulikuwa na sanduku la mbao ambalo Musa alitengeneza. Ndani yake mlikuwa na nakala mbili zaidi za mawe za agano, yaani amri kumi. Juu ya sanduku hilo ilikuwa ni dhahabu safi na makerubi mawili walionyoosha mbawa zao kuelekeza kila moja. Mungu alionyesha uwepo wake kwa watu wake katika nuru kuu iliyokuwa juu ya sanduku chini ya mbawa za makerubi.
Mbele nje ya hema, kulikuwa na madhabahu kubwa ambapo watu walitoa dhabihu kwa Mungu. Na pia kulikuwa na karai ya maji ili makuhani wangenawa mikono na miguu kabla ya kutoa dhabihu.
Kila kitu kilikuwa maridadi na kitakatifu. Mungu akasema, yeyote isopokuwa makuhani, akigusa vitu vitakatifu, atakufa. Kwa hivyo kulikuwa na ukuta wa chandarua uliozunguka hema kwenye nguzo za mbao.
Kisha Mungu akamwambia Musa amweke wakfu ndugu yake Haruni, awe Kuhani Mkuu, wana wa Haruni wawe makuhani chini yake, na wazao wengine wa Lawi ili kusaidia katika baadhi ya kazi za hema la kukutania, na kuibeba watu walipokuwa wakisafiri.
Kutoa Dhabihu
Kila asubuhi na jioni, makuhani walimwuua mwana kondoo asiye na waa, kisha wakamchoma juu ya madhabahu. Pia, waliingia chumba cha kwanza cha hema, yaani pahali patakatifu, ili kuchoma uvumba na kuwasha taa mbele ya Mungu.
Mtu alipovunja sheria za Mungu alileta mwana kondoo au mbuzi kama dhabihu ya dhambi. Kuhani alimchinja mnyama huyo na kumwaga damu yake juu ya madhabahu. Hii ndiyo sababu Mungu alisema, “Usile nyama pamoja na damu. Uhai wa mwili u katika hiyo damu, nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”
Kulikuwa na aina kadhaa za dhabihu, lakini Mungu angeruhusu tu, wanyama fulani kutolewa dhabihu. Hawa wanyama walikuwa ni ng'ombe, kondoo, mbuzi, au njiwa. Na kila mmoja alipaswa kuwa mkamilifu, asiye na dosari, asiwe mgonjwa, mzee, au mnyama aliyeharibika…ila bora zaidi. Dhabihu zingine za wanyama hazikukubaliwa na Mungu na hazingeondoa dhambi. Njia pekee ya kuondoa dhambi za watu, ilikuwa jinsi Mungu alivyowatengenezea.
Siku ya Upatanisho
Mara moja kila mwaka, katika Siku ya Upatanisho, kulikuwa na dhabihu maalum.
Kwanza, kuhani mkuu alichagua mbuzi wawili, mmoja wa kuua na mwingine wa kumfukuza. Baadaye, Kuhani Mkuu alimtoa fahali na aliingia nyuma ya pazia katika Pahali Patakatifu Zaidi, katika uwepo wa Mungu. Alinyunyizia damu juu ya kifuniko cha dhahabu cha sandaku, ili kupatanisha kwa dhambi zake kwanza.
Nje alimchinja mmoja wa mbuzi na kuenda nyuma ya pazia tena na kunyunyuzia damu ya mbuzi huyo juu ya kifuniko cha dhahabu cha sanduku. Hii ilikuwa ni kwa kupatanisha kwa dhambi ya Wana Israeli. Mwishowe, alimleta yule mbuzi aliye hai na kuweka mikono yake juu ya kichwa chake na kuungama dhambi zote za Waisraeli.
Atakuwa anaweka dhambi zao juu ya kichwa chake. Baadaye, mtu alichukua mbuzi huyo jangwani mbali sana na kambi, ili asiweze kurudi kamwe. Na mbuzi yule alizibeba dhambi za watu juu yake.
Kutotii
Licha ya yote, watu bado hawakumtii Mungu, hata wana wawili wa Haruni ambao walikuwa makuhani. Walijaribu kufukiza uvumba kwa njia yao, si kwa njia ya Mungu. Kwa hiyo Mungu akatuma moto kutoka mbinguni na kuwaua pale ndani ya hema. Kwa sababu hawakumheshimu Mungu na utakatifu wake, Haruni baba yao hakuruhusiwa kuomboleza kwa ajili yao.