CBS Stories

Swahili Stories

Kuwalisha Watu Elfu Tano

Marko 6:30-44, Matayo 14:14-21, Yohana 6:1-14, Luka 9:10-17

Siku moja Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi wake. Kwa sababu watu wengi walikuwa wanakuja kwake hawakupata nafasi ya kupumzika au kula.  Kwa hivyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twende peke yetu mahali pengine kupumzika.” Wakaingia merikebu kuvuka ziwa kuenda mahali pa tulivu. Lakini watu wengi waliwatambua wakawafuata kwa miguu wakawatangulia.  Yesu alipofika mahali aliwaona umati akawanoea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji. Akaanza kuwafunza mambo mengi.

Jioni ilipofika wanafunzi wake wakamjia wakisema, “Hapa ni nyikani, na usiku umekaribia. Waruhusu watu waende katika vijiji vinavyotuzunguka, wajinunulie kitu cha kula.” Lakini Yesu akawajibu, wapatieni ninyi chakula.” Wakamjibu, “Jambo hili litachukua mshahara wa mtu wa miezi minane! Je, tutumie gharama hii yote kwa mikate tu?” Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Walipojua wakasema, “Mikate mitano na samaki wawili.”

Yesu akasema, “Leteni hapa.” Kisha Yesu akawaelekeza wawaketishe watu kwa makundi. Akachukua ile mikate mitano na samaki wawili na akiangalia mbinguni akashukuru Bwana na kuigawa chakula. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawape watu. Pia akagawanya wale samaki wawili kwao wote. Wote wakala na kutosheka, na wanafunzi wakakusanya vikapu kumi na viwili: vipande vya mikate na samaki. Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano. Na watu wakashangaa! Wakaanza kusema, “Kwa kweli huyu ni Nabii ambaye amekuja ulimwenguni”.