Walipokuwa wangali wanaongea kuhusu taarifa kutoka ndugu za Emaus, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao akawaambia, “Amani iwe kwenu.” Walishangaa na kuogopa sana, wakifikiri wameona pepo. Yesu akawaambia, “Mbona mnafadhaika, na kwa nini mna shaka moyoni mwenu? Ebu tazameni mikono na miguu yangu. Ni mimi mwenyewe! Niguzeni mwone; pepo hana mwili na mifupa jinsi nilivyo.” Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. Na wakiwa wangali hawawezi kusadiki kwa sababu ya furaha na mshangao, akawauliza, “Je, mna chochote cha kula? Wakampa kipande cha samaki aliyepikwa, akachukua akala mbele yao.
Akawaambia, “Hili ndilo nililowaambia nilipokuwa ningali nanyi. Kila jambo lililoandikwa kuhusu mimi katika sheria ya Musa, manabii, na zaburi lazima litimie.” Kisha akafungua akili zao ili wayafahamu maandiko. Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na kufa kisha atafufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu, na toba na msamaha wa dhambi utahubiriwa katika jina lake kwa mataifa yote kuanzia Yerusalemu. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. Ninaenda kuwatumia kile Baba ameahidi; lakini kaeni mjini hadi mtakapovalisha nguvu mpya kutoka juu.”
Alipokuwa amewaongoza hadi eneo la Bethany, aliinua mikono yake akawabariki. Alipokuwa akiwabariki, aliwaacha akachukuliwa juu hadi mbinguni. Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu na furaha kuu wakakaa kwa muda katika Hekalu wakimsifu Mungu.
Huu ndio mwisho wa hadithi.