CBS Stories

Swahili Stories

Eliyah na Manabii wa Baali

1 Wafalme 18

Eliya alikuwa nabii mkuu ambaye Mungu alimtuma kwa ufalme wa kaskazini wa Israeli katika siku za mfalme mwovu, aliyekuwa akiabudu sanamu, jina lake, Ahabu. Kwa sababu ya dhambi ya Israeli, Eliya alitabiri ukame, na Mungu akasimamisha mvua yote kwa miaka mitatu. Wakati huo Eliya alijificha mbele ya Ahabu. Mwishoni mwa miaka mitatu bila mvua, Eliya alijitokeza tena na kujionyesha kwa Mfalme Ahabu.

Ahabu akamwona Eliya akasema, Je ni wewe ewe mtaabishaji wa Israeli? Eliya akajibu, sio mimi niliyewataabisha Israeli, bali ni wewe na nyumba ya baba yako kwa kuwa mumeziacha amri za Bwana, na kuabudu sanamu Baali. Kisha Eliya akasema, “Wakusanyeni Israeli wote kwenye Mlima Karmeli, nasi tutaona ni nani aliye Mungu wa kweli, Yehova au Baali.

Katika siku iliyochaguliwa, Mfalme Ahabu alikuwa huko na manabii mia nne na hamsini wa Baali. Na Israeli wote wakakusanyika katika Mlima Karmeli. Eliya alisimama peke yake kwa ajili ya Bwana. Eliya akawaambia watu, “Acha nitoe dhabihu bila moto.

Hebu manabii mia nne wa Baali pia watoe dhabihu bila moto. Mungu atakayejibu kwa moto ndiye Mungu wa kweli.” Watu wote wakasema, “Ndiyo! Huo ni mpango mzuri!”

Basi, asabuhi iliyofuata, manabii mia nne wa Baali waliomba, “O Baali! Utusikie! Uutume moto!” Walilia mpaka adhuhuri na hakukuwa na chochote kilichofanyika. Saa sita, Eliya aliwadhihaki akasema, “Pengine Baali analala! Au labda alisafiri. Pazeni sauti!” Basi manabii wa Baali walianza kuruka na kucheza ngoma na kupiga kelele hata kujikata wenyewe kwa visu mpaka damu ikamwagika. “O Baali! Tusikie! Tuma moto!” Oh Baali!, Tuskie! Tuma moto! Lakini, jioni ilipofika, bado hakukuwa na chochote kilichofanyika.

Kisha Eliya akasema, “Tosha! Sasa ni wakati wangu!” Eliya akajenga madhabahu kwa Bwana kwa kutumia mawe kumi na mawili. Akamchinja fahali na kumweka juu ya madhabahu. Kisha akachimba mtaro kuzunguka madhabahu na akawafanya wanaume kuchukua mitungi kumi na miwili ya maji na kumwagilia dhabihu hadi yakamwagika na kujaza mtaro. Basi Eliya akaomba akisema, “Ee, Mungu. Jionyeshe wewe ndiwe Mungu nami ni mtumishi wako.” Punde si punde, moto ukashuka kutoka mbinguni na ukachoma dhabihu kabisa pamoja na kuni na hata mawe na maji.

Kisha watu wote wakashangilia, “Bwana ni Mungu!” “Bwana ni Mungu!” Kisha Eliya akasema, “Wachukue manabii wa Baali na kuwaua. Baada ya jambo hili, Mungu alileta mvua tena.