CBS Stories

Swahili Stories

Chakula cha Mwisho

Luka 22:1-22; Matthayo 26:26-30; 1 Wakorintho 11:23-25

Hii ni hadithi ya meza ya Bwana ya Mwisho.  Wakuu wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumwua Yesu. Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu ili amsaliti. Kwa hivyo Yuda alikwenda kwa viongozi wa Wayahudi na kukubaliana nao kumtoa Yesu kwao kwa kulipwa fedha fulani.

Na sasa ulikuwa wakati wa sherehe za pasaka naye Yesu alikuwa amewatuma wanafunzi wake kuandaa sherehe hiyo.  Akasema, “Nimetaka sana kula chakula cha pasaka nanyi kabla ya kuteseka. Sitakula tena mpaka wakati wake kamili utakapotimizwa katika Ufalme wa Mungu. Lakini mmoja wenu hapa atanisaliti.  Mwana wa Adamu atakufa jinsi Mungu alivyoamua lakini ole wake mtu anayemsaliti!”

Wanafunzi walihangaika na kuanza kumwuliza, “Bwana siye mimi, ni kweli? Bwana ni nani?” Yesu akawajibu, “Ni yule nitakayempa kipande hiki cha mkate.” Alikichovya kipande hicho katika mchuzi kisha akampa Yuda Isakariote akimwambia, “Nenda haraka, ufanye utakavyo.”  Licha ya kuwa giza Yuda alipokula ule mkate aliondoka.

Baada ya kula chakula cha pasaka, Yesu alichukua mkate, akashukuru, akaumega akawapa wanafunzi akisema, “Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” Katika njia hiyo, Yesu akakichukua kikombe akasema, “Hili ndilo agano langu jipya katika damu yangu ambayo itamwagika kwa ajili ya msamaha wa dhambi.”

Baada ya kushiriki katika mkate na kikombe  na baada ya Yuda kutoka nje, Yesu alisema “Ninyi nyote mtanitoroka. Lakini baada ya kufufuka, nitakutana nanyi katika Galilaya.” Nao wanafunzi wakahuzunika sana.  Baada ya chakula cha pasaka kuisha waliimba Zaburi. Kisha wakaondoka mji wa Yerusalemu kuenda kwenye bustani katika Mlima wa Mizeutuni pamoja.

Huu ndio mwisho wa hadithi.